Recent Posts

Mimi ni mwana Blogu au mimi ni mwana  globu?

Je blogu yangu ni blogu au globu?

Tafakari jadili.

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, September 27, 2012 0 comments

Kwanza,haiwezekani habari moja iwe kichwa cha habari katika magazeti,luninga au blogu.Haiingii akilini aina ya habari moja kuwa kicha cha habari katika vyombo vyote vya habari na ukisoma zaidi habari hizo zinakizana.

Namwamini Mungu,mwingi wa rehema,habari yake huwezi kucopy na kupaste kama wengi tunavyofanya,namwamini Mungu,mweza wa vyote.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, July 29, 2012 0 comments

Kama wewe ni mzuri kwanini hujaolewa? Na kama unajijua wewe ni mbaya kwa nini unatumia MAKE UP?

Swali?

Naomba jibu.

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, July 26, 2012 3 comments


"Bingi man say come, when sellasie call you you must come" with an opening line like that, how will this song ever go stale? Hurry up and come or Bingi man shall wash you away.

 

MWENYE SIKIO NA ASIKIE.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments


http://simon-kitururu.blogspot.com/
Nimeipenda sana hii picha ya Mtakatifu Simon Kitururu,pia nimeipenda kutokana na Mtakatifu kuinyooshea kidole akimaanisha AFRIKA.

Pia nimeipenda hii picha na kumkumbuka Nabii Lucky Dube katika wimbo wake different colours ONE PEOPLE.

Amani.

Posted by nyahbingi worrior. 1 comments

Unaweza sikia kinadada wa nyumbani hawalalamiki pindi wanapoachiwa watoto wadogo siku nzima wawaangalia wakati wazazi wakitoka kwenda kutafuta ugali.Mtoto hasumbui na ukimpatia hato sumbua kamwe.

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, July 21, 2012 1 comments

Ndugu zanguni,niko kwenye RETREAT maeneo flani hivi Dar,ni chimbo la ukweli,kweli wafanyabiashara hawana mchezo.Hili Chimbo ni babkubwa,vyumba ni babkubwa,chakula babkubwa na MILANGO NI BABKUBWA.

Jamani,jana baada ya kikao,nilikwenda chumbani,hivi vyumba vinafunguliwa na kadi,baada ya kufungua kwa kutumia kadi yangu,niliingia ndani ili niweze kulala lakini nilipofunga mlango kwa ndani na kisha kucheki kama nimefunga,mlango ulifunguka,kila nikijaribu kucheki kwa kufungua,mlango unafunguka.

Nilitokana kwenda kumcheki mhudumu,nikamweleza,akanijibu bwana hii milango ukifunga kwa ndani,kwa aliye nje hawezi mkufungua lakini wewe uliye ndani unaweza kufungua.

Mnaona,mambo haya,sasa kama bongo ni hivi je kwa kina mtakatifu?

Posted by nyahbingi worrior. 1 comments

Swala la mtihani ni kujipima uwezo,sasa mwanafunzi anapotumia matango pori sijui anamwongopea nani.

Posted by nyahbingi worrior. Friday, July 6, 2012 0 comments


Tukio hili nalikumbuka,nakumbuka siku ya ubarikio wangu,Moshi, Sango.Hapa Mzee, Profesa Winnyston Njelekiro Ringo ananikabidhi zawadi ya BIBILIA.

R.I.P Profesa W.Ringo.

Posted by nyahbingi worrior. Tuesday, July 3, 2012 2 comments

 Kwa mbali pipa la mbege linaonekana huku wazee wa UKOO wa Ringo wakiburudika.
 Hapa nakabidhiwa ndoo ya MBEGE na wajomba kama mila na desturi inavyoeleza.
Hapa,meza kuu.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo