Recent Posts

Swali
Kaka,samahani umewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watu wangapi katika maisha yako?

wa kwanza.
Mimi nakumbuka nimewahi kuwa na mahusiano na mabinti kumi tofauti tofauti tangia kidato cha kwanza.Nakumbuka nilipokuwa kidato cha kwanza nilikuwa na mahusiano na binti ambaye alikuwa kidato cha nne lakini shule tofauti kwani tulikuwa majirani nyumbani.Agnes alinipenda sana,alinijali sana na tulikaa kwa amani na upendo hadi nilipofika kidato cha pili mwishoni.Sababu ya kuu ya kutengana ilikuwa niendelee na masomo yangu vema na nifaulu vema.Leo hii Agnes kaolewa Ujerumani na anawatoto wawili.

Wapili nilipenda kumwita Trice,nilikutana naye kidato cha tatu mwanzoni kabisa.Alinichanganya na alinipenda kwa utundu wangu.Alikuwa mcheshi sana na mvumilivu kupita kiasi.Trice nilikaa naye hadi tulipo maliza shule.Kwasasa Trice kaolewa Ubelgiji na bado hajapata mtoto.

Watatu ni lili,lili kwa sasa yuko marekani,tulidumu takribani miaka miwili.Anawatoto wawili tena mapacha.

Wanne anaitwa Sarah,sarah tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja..kwasasa sijui yuko wapi kwani mara ya mwisho alikuwa uk.

Watano anaitwa Sozy,Sozy tulidumu kwa nusu mwaka..kwasasa yupo na anaendelea na maisha yake.

Wa sita anaitwa Lei,Lei tulidumu kwa nusu mwaka....kwasasa anaendelea na masomo yake.

Wa saba anaitwa T.G. Kati ya wote TG tulidumu tu mienzi mitatu kisha tukashindwana au kukubaliana na maamuzi yetu.Kwasasa yupo na maisha yake.

Wa nane baada ya kutengana na TG tulirudiana na Lei kwa mwenzi mmoja ili kupoteza hisia zangu kwa T.G.

Wa Tisa yupo,nitakutana naye karibuni kwani nimemwalika chakula cha mchana jumamosi ya 28/11/2009.

Kwa kweli na weka mambo wazi,kati ya hawa Tisa kila baada ya mausiano kuvunjika nilikuwa najituliza na wale wanaouza(malaya) lakini nilikuwa na tumia kinga na kumbukumbu ninazo.

Je wewe msomaji umewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume au wanawake wangapi hata kama umeoa au kuolewa?

Kati ya hawa wote,niliyempenda sana ni Trice na bado nampenda sana.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, November 25, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo