Recent Posts

tulipokuta mara ya kwanza,
upendo ulitawala kwanza
sikuamini uliponiambia kwanza,
nilithamini uliponena kwanza,
hisia haziku sita kwanza,
kwanza ulikuwa mwanzo wa kwanza.

nililala kama mfalme,
niliota ndoto kama mfalme,
uso ulikuwa na furaha kama mfalme,
sikudhania nitaangamia mfalme.

sasa najuta kwanza,
nahisi tusingekutana kwanza,
natamani mwanzo usingekuwa kwanza,
naumia,
nikikuwaza naumia,
sina ladha ya chakula,
najitahidi kukuacha kwanza,
najitahidi kukuondoa akilini kwanza.

Posted by nyahbingi worrior. Monday, November 2, 2009

4 comments

 1. Serina anasema:
 2. Majuto majukuu!

   
 3. Majuto ni Mjukuu Serina.

  Huyu Majuto?

   
 4. Serina anasema:
 5. Nitajuaje?
  s.

   
 6. utajuwa tu serina.

   

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo