Recent Posts

Kwanini vijana wengi wanapenda kusikiliza muziki wenye ujumbwe wa mapenzi?

Kuna wakati nabii Robert Nesta Marley alikuwa akipiga tungo zenye kujaa mapenzi kupita kiasi,basi waalimu wake nabii mortimmer planner na Ras Lyood WALIMWITA NA KUMWAMBIA NABII bOB mapenzi hayana msingi katika maisha ya mwafrika wakati bado wanakandamizwa na kunyimwa haki zao za msingi.

Sasa basi tuangalie wasanii wetu wa leo,hawana jipya licha ya kuimba mapenzi mapenzi kila siku mpya ya babylon by bus.Hivi wasani wetu wa leo wana waalimu kweli?

Kwamsanii,je unapata nini pale unatoa ujumbe wa kumtukuza mwanamke au mwanauwe?Tungo nyingi za leo zinawapotosha watu au jamii,wasikilizaji wa tungo hizo hulemaa katika maisha ya kuabudu mwanamke au mwanamke.

Kwa vituo vya habari au vyombo vya habari.Mimi kwa mtazamo wangu ningepiga marufuku kupigwa kwa wimbo au nyimbo zozote zile zinazo zungumzia mapenzi.Wasanii wetu inabaidi mwamke na wasikilizaji inabidi tuamke tuache kusikiliza hizo tungo za mapenzi.

Nini cha kusikiliza basi?
Kwanza naamini masikio yetu na akili zetu zinapenda kusikiliza tungo za UKOMBOZI za mtu mweusi.Nyimbo zilizo sheheni HAKI,KUJITAMBUWA,UPENDO n.k.

Posted by nyahbingi worrior. Friday, December 18, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo