Recent Posts

Afande sele aliwahi kusema sio wote lazima tuwe wasanii,ni vema wengini tubaki mashabiki.

Sio wote tuwe wanablogu,ni vema wengine tuwe wasomaji,wachangia maoni n.k

Siku hizi ukiwa na digital kamera basi wewe ni mwanablogu.

kwanini tunatumia nguvu ya kamera?

Je!tunatumia kamera ipasavyo?

Blogu zimejaa picha za starehe wakati tunakiu ya habari?

Nauliza tena,Blogu ni nini?

Posted by nyahbingi worrior. Monday, July 26, 2010

3 comments

 1. chib anasema:
 2. Ukiingia kwenye mtandao wa world of blogs, utakuta wameweka makundi mengi ya blogu, hakika ukiingia hapo utajua maana ya blogu, kwani zina mitazamo mingi zaidi ya 20. Inategemea wewe unaangalia blogu kwa mtazamo upi. Ni sawa na magezi na vijarida

   
 3. Fadhy Mtanga anasema:
 4. Wacha ziwe nyingi tu. Ni uhuru wa kila mtu kuzungumza. Lengo la kwanza kabisa la blog ilikuwa kuifanya online diary. Sasa sidhani kama watu wanawekewa mipaka kuandika kwenye diary zao. Wanaoweka picha sawa. Wanaoandika vimbwanga sawa. Wanaofanya nini sijui sawa.

  Uwanja huu mpana unampa uhuru msomaji kuamua asome wapi na nini. Hata kungekuwa na blog hamsini tu dunia nzima, bado mie nisingeweza kuzisoma zote. Hivyo sioni tatizo na idadi wala yaliyomo. Ninao uhuru.

   
 5. SIMON KITURURU anasema:
 6. Mmmmh!

   

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo