Recent Posts

Kama mtu amefiwa au kagongwa na gari,au kalazwa,kuna neno moja tu la kusema nalo ni Pole.Hii tabia yakusema ni kazi ya shetani kwakuwa flani kafa haifai,Mungu ndiye anayetoa na vilevile ndiye anayetwaa sasa huyu shetani anatokeo wapi?

Umeambiwa Nyahbingi worriors kafa,sema pole,haya mambo ya kusema ooohhhh my god this cant be,nilikuwa naye jana,namdai,ananidai yaishe.

au Mzee wa mawazoni unasemaje?

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, March 24, 2011

2 comments

 1. Anonymous anasema:
 2. Yote ni mapenzi ya mungu, mengine ni sababu, siku ikifika haikosi sababu!

   
 3. SIMON KITURURU anasema:
 4. Nakubali usemalo. Ila binadamu wamezoea wasiyoyapenda kumsingizia SHETANI ! Ingawa mengi wayapendayo na matamu kama ngono , anasa nk.- yasemekana ni ya shetani vilevile ila kwa kuwa ni matamu huwa hawamlalamikii shetani kwa hayo.

  Ila kujinyima, kifo , au tu MAGONJWA labda ni mambo magumu kwa wengi kumsingizia MUNGU huyohuyo asifiwaye kwa kumuotesha Babu wa Loliondo atoe kikombe kwa shilingi mia tano tu ili wagonjwa wasiteseke.

  Wengi wetu ya MUNGU na maumivi huwa hawayaoanishi.:-(

   

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo