Mtakatifu au mzee wa mawazoni.
Nachukuwa nafasi hii nikiwa hapa Afrika kukujulisha ya kuwa kwa kipindi sasa nimekuwa siwezi kufunguwa blogu yako.Nimekuwa nikijaribu kila wakati lakini baada ya kubofya linki yako,inafungukuka kwa kuleta kurasa yako kisha inapotea.
Sasa sijui ni computer yangu itakuwa na virus au nini.
Nakuomba unisaidie katika hili kwani siwezi kupata ya mawazoni.
Amani iwe nasi sote.
Nyahbingi worrior.
Friday, April 22, 2011
Worrior
Nimefurahia kusoma leo mara ya kwanza BLOG yako, pia na mawazo yako, hasa kwenye ABOUT-ME yako sasa nakunukuu:
“DIS BLOG SHALL BE CALLED BORING,STUPID,SENSELESS. DIS BLOG IS WATCHIN U TRYING TO MAKE SENSE FROM DIS BLOG.”
Kiswahili chake ni nini? Je, mimi naweza kutafsiri?
Yaani kweli BLOG yako [YAMLAZA MTU DAMU, NI YENYE UPUMBAVU MTUPU NA UJINGA? NA BLOG YAKO HII IMENIKODOLEA MIMI MACHO KAMA NINAVYOANDIKA]?
Basi nitairudia tena. Napenda kuangaliwa. Labda BLOG yako imenipenda, sio?
Kuhusu Simon Kitururu na BLOG yake:
Chunguza sana kampyuta yako uone kiwango cha plastiki. Kama plastiki ni nyingi mno (kama hii ya kwangu), hakika kampyuta hiyo inaweza ikawa inayayuka kila ukimwendea Simon Kitururu kwani BLOG yake ni moto kabisa! Kwa kawaida mimi nikitaka kumwendea Simon, nafungua BLOG yake nikiwa tayari LAPTOP/kampyuta yangu nimekwishaweka juu ya BLOCK ya barafu!
Kwa hiyo: BLOG=BLOCK!
Mkuu Goodman,umenipata,umepatia.