Recent Posts

Tupende tusipende lazima wengine tubaki kuwa wasomaji au wachambuaji wa blogu.

Kwasasa kunauulazimu wa kuwa na  MHARIRI katika blogu zetu.

COPY NA PASTE inazidi kukuwa kwa kasi,wanablogu tunacopy na kupaste kupita kiasi hadi inakera yani inatia kichefuchefu,haiwezekani habari moja unaikuta katika blogu zaidi ya kumi alafu tunajiita wanablogu.

BIRTH day ndio zinachukuwa vichwa vya habari siku hizi,wanablogu wanaweka habari za birth day huku mamia ya watu wanataabika,wanaweka picha zinavyoonyesha watoto wao wanavutimiza mika kwa kuzima mishumaa.

Blogu za Ngono,hizi ndio zinachua kasi tena.Hivi unapotizama hizi picha za ngono  unapata raha gani?

Blogu za MAWAZI,hali ya fedha imekuwa ngumu,maisha yamepanda lakini nashangaa kwa baadhi ya blogu kuweka habari za mavazi.Katika hali hii ngumu ya maisha nani anahitaji mavazi ya fashion?


BLOGU na Matangazo,sasa hivi mwanablogu anajitahidi kupata matangazo katika blogu yake ili apate angalua vijisenti nasio tena umuhimu wa habari katika blogu yake.


Jamani,wengine tubaki wasomaji.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, June 27, 2012

1 Responses to Wengine tubaki kuwa wasomaji wa blogu.

  1. emu-three anasema:
  2. Mkuu umetia neno, na kama ujuavyo ukweli huuma hata kama ni kidonda, ndio maana hujaona mtu akinena lolote, kama ungenena umbeya na picha za nanihino, na ....basi ungeona koments kibao, lakini wapiii....
    Usijali mkuu tupo pamoja

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo