Recent Posts

Ndugu zanguni,niko kwenye RETREAT maeneo flani hivi Dar,ni chimbo la ukweli,kweli wafanyabiashara hawana mchezo.Hili Chimbo ni babkubwa,vyumba ni babkubwa,chakula babkubwa na MILANGO NI BABKUBWA.

Jamani,jana baada ya kikao,nilikwenda chumbani,hivi vyumba vinafunguliwa na kadi,baada ya kufungua kwa kutumia kadi yangu,niliingia ndani ili niweze kulala lakini nilipofunga mlango kwa ndani na kisha kucheki kama nimefunga,mlango ulifunguka,kila nikijaribu kucheki kwa kufungua,mlango unafunguka.

Nilitokana kwenda kumcheki mhudumu,nikamweleza,akanijibu bwana hii milango ukifunga kwa ndani,kwa aliye nje hawezi mkufungua lakini wewe uliye ndani unaweza kufungua.

Mnaona,mambo haya,sasa kama bongo ni hivi je kwa kina mtakatifu?

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, July 21, 2012

1 Responses to Kutokujua si ujinga,ujinga ni kutokuuliza.

  1. Yasinta Ngonyani anasema:
  2. Nakubaliana nawe 100% kuuliza si ujinga na hapo ndipo ule msemo usemao aulizaye hujua mengi...

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo