Recent Posts

si maneno tu,
bali hata vitendo.

amini nachokwambia,
kitokacho kinywani mwangu,
uwe na amani.

usiutese moyo wako,
kwa yako mawazo,
u we na amani.

nilikutamkia nakupenda,
si kulazimishwa kukupenda.
u we na amani.

umbali wetu usiwe kisingizio,
ukaribu wetu usiwe kigezo,
uwe na amani.

mengi yasemwa,
wengi wateswa,
wakutesaho watazidi kukuteta,
uwe na amani.

si kucheka na kunena,
si wapitao wote nawatamani,
uwe na amani.

amani iwe nawe,
amani iwe nasi,
amani ndani ya miyoyo yetu,
tuwe na amani.

Posted by nyahbingi worrior. Friday, October 9, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo