Recent Posts

Ni mkombozi wa wawakombozi,
CHE,
Ni jasiri wa kupita siri,
CHE,
Vijana wanakuvaa,
CHE,
Wengine hawakutambui,
CHE,
Wachache twakutambua,
CHE,
Rafiki yako bado yu jasiri na nguvu tele,
CHE,
Wabepari bado wanatikisika wakisikia sera zako,
CHE,
waslimu huko uliko,
CHE,
Msalimu Mwalimu Nyerere,Jomo Kenyatta,Dedan Kimathi,Moringe Sokoine,Profesa Walter Roodeny,Patrice Lumumba,Steve Biko,Haile Selassi I,
CHE,
Usisahau kuwasalimu manabii waliotumia nyimbo za REGGAE kueneza ukombozi,
CHE,
Nakukumbuka CHE.

Posted by nyahbingi worrior. Monday, November 30, 2009

2 comments

  1. Mwezi uliopita kulikuwa na maandamano hapa chuoni kwetu yaliyokuwa yameandaliwa na wanafunzi wa nchi za Latin Amerika. Walikuwa wanaandamana kuonyesha kwamba CHE alikuwa ni GAIDI aliyeua maelfu ya watu na kwamba hastahili kuitwa "mwanamapinduzi".

    Niliwasikiliza, wakanipa fulana yenye picha ya CHE lakini imepigwa alama ya eksi nikaondoka zangu....

     
  2. NABII hakubaliki nyumbani.Kwa yule aminiye Che ni mkombozi basi aendelee kufanya hivyo.

    amani kaka.

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo