Recent Posts

nakiri ninayo,
mapungufu ninayo,
hakuna aliye kamilika.

nishik mkono ili nikamilike,
bega kwa bega na mapungufu kuyarekebisha,
naelea baharini,kimo kimenizidi.

nateseka kwa kukuweka kichwani,
mawazoni,
yote mapito,njia mpito.

anayenipenda simpendi,asiyenipenda nampenda,
mapenzi kizungumkuti,
nikubali na mapungufu yangu,kuyarekebisha yahitaji muda.

mwenzangu wakamilika,
heri na kupa,mafanikio mema maishani,
umwaminiye azidi kukubariki,
ni safari tu ya asiye kamilika.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, November 18, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo