Recent Posts

Mfungwa hutoka kifungoni,
na kuwa huru tena,
sitaki tena lalama,
sitaki lalamika tena,
sitaki kunungunika tena,
sitaki lia lia tena,
sitaki,sitaki,sitaki.

nimecho mwezenu,
mwenzangu ala raha na mabuzi,
acheza disko kama kicheche,
nilie kwa nini?
nijikwaze kwa nini?

hakuna wa kunipa raha ila mwenyewe,
sisubiri raha kwa mwingine,
naamini ntampata wangu wa moyo,
haijalishi miaka mingapi,
imetosha,imetosha,imetosha,imetosha.

gidamu na kaza,
buti na kaza,
Serina asante kwa mashairi,
nasonga mbele najuwa si mwenyewe,
IMETOSHA,IMETOSHA,IMETOSHA.

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, November 5, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo