Recent Posts

Mimi siamni katika misemo yao yakwamba ATASHUKA JUU MAWINGUNI KUJA KUCHUWA KANISA LAKE.....lipi?Haya yote walitaka tuachane na imani za MABABU zetu zenye nguvu kuliko zao basi wakaja na misemo yao ya NJIA ILE NI NYEMBAMBA IENDAYO UZIMANI(uhuni)

Kwanini watu wanakwenda katika nyumba za ibada?na kwanini ni siku moja tu watu ndio hukumbuka kwenda kutubu dhambi zao?(siku ya jumapili kwa wale wakristo)Nilipata muda kuzungumza na vijana walokole wanavyojiita siku hizi.Wao wanajigamba ufalme wa mbinguni ni wao,wanajigamba na madhehebu yao yawafundishayo imani zao.

Wengi wetu tunaogopa kifo,wengi tunataka kwenda mbinguni lakini hakuna hata mmoja anataka kufa kwa ajili ya jirani yake.Kwa nini?Kama sio unafki?

Kifo kiko pale pale hata kama uhudhurie ibada miaka nenda rudi lazima UFE kwasababu hiyo ndio DESTINI YAKO/YANGU.

Mimi binafsi wakati naabudu humwambia Mungu kama ni kwamapenzi yako umeona wakati wangu ni leo,asubuhi ya leo au jioni ya leo unataka kunichukuwa,nichukuwe kwani niko tayari.

Wengi bado tuna ukungu wa kuomba kuishi miaka 100 na kuendelea wakati uwepo wapo hapa duniani ni mateso kwa wengine,mateso kwa maskini.

Tukubaliane kwa kuto kukubaliana:KUFA KUPO.UWE TIYARI.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, November 1, 2009

2 comments

  1. mbona mimi siamini kama kuna kifo na nasema binadamu hafi bali huacha tu mwili?

     
  2. kaka,mwili unabaki lakini roho inakwenda wapi?mwili unazikwa LAKINI ROHO hubakia HAI.

    dUH?

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo