Recent Posts

Nikupe ni nini ewe Mungu wa miungu,
umenipa UJASIRI wa ajabu,
umenitoa pale nilipokwama,
umenishika mkono kila siku yako mpya,
nakupenda ewe Mungu wangu.

walio wachafu wanakunena,
wananinena kwa kuwa na kusifu na kukuabudu,
wewe ni Mungu wangu,
mwenza yote,
nakupenda mungu wangu.

siwezi kuhukumu,
nawabariki maadui wangu,
nawapenda walionidhulumu,
nawatakia heri mlioninyanyasa,
wewe ni MUNGU WA KWELI.

Bado nafanya kazi ilionipa,
sitochoka kuwaiita ndugu zetu warudi Afrika,
ingawa wengi wamelewa ugenini,
hawataki kurudi tena nyumbani,
macho yao yamefunikwa na ukungu wa mazuri yao.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, November 1, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo