Recent Posts

jumuwata itafufuka,
kama siku ya tatu alivo fufuka na kupaa juu mbinguni,
nitasimama mkono wa kuume wa mwenyekiti,
kama alivokaa mkono wa kuume katika kiti cha enzi,
jumuwata itafufuka.

sikieni sauti ya nyikani iwaitayo enyi wanablogu,
simon sikiliza kwani ukatibu unao,
msangi nawe uenyekiti wakutazama,
da mija mweka hazina tunataka mahesabu,
jumuwata itafufuka.

kwenu,
wafuasi mlio hai,
imani yenu itaifufuwa,
pasipo mimi kupiga mayowe,
jumuwata itafufuka.

kwetu mwalimu Ndesanjo,
funguo katupa,
gari kalinunuwa,
kufundisha kafundisha,
je atakuwa nasi kila siku?
je imani yetu iko wapi?
jumuwata itafufuka.

na sasa tuungane,
makosa tuyakubali,
kuwajibika tujitolee,
jumuwata itafufuka.

ugaibuni nitakwenda,
bize nitakuwa,
na jumuwata kuisahau,
maisha huku mazuri,
jumuwata yanisaidia nini?
wapiga kelele mlioko BONGO,
mwataka jumuwata?
bei ya DOMAIN mwaijua?

kesheni mkiomba
niko kwangu barafuni,
na poteleambali na jumuiya yenu,
kodi nalipa,
bado mwanizingua na jumuwata yenu?
ya nini?
nilishapata nilichokitaka.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, January 13, 2010

2 comments

  1. Mija Shija Sayi anasema:
  2. Luihamu usikate tamaa Luihamu.

     
  3. Da Mija sito kata tamaa naamini ipo siku mambo yatabadilika.

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo