Recent Posts

Funguwa hapa kwa mwanamke wa shokahttp://damija.blogspot.com/ kisha tujadili maoni ya KATIBU,MTAKATIFU SIMON na kaka BWAYA kuhusu JUMUWATA.

MAONI YA KAKA BWAYA...
Baba Mtakatifu, nadhani juhudi ulizozifanya zinatosha. Mimi ni shahidi nambari moja. Kwa sasa nadhani inatosha kabisa kusema 'sina'. Baada ya kuchunga sana sakata hili la JUMUWATA nilichokibaini ni hiki. Hatuwezi kufufua kulichokufa. Uwezo huo (wa kumrudishia uhai mfu anao mwenyezi Mungu pekeyake.)Na tunaweza kudhani tunafufua wakati tunaua kabisa. Halafu huwezi kufufua kisicho na wafuasi. Utajikuta unafia kwenye maiti.Du nisiendelee sana. Nikiri kwamba juhudi za Katibu nilizitambua tangu awali na bado nazitambua. Ila shida ni kifo cha kinachosumbukiwa. Suala la kimaumbile. Luihamu:Natambua uchungu ulio nao na ufufuzi wa hiki kilichojulikana kama JUMUWATA. Lakini kwa jicho la ndani, naomba tupime upya. Tunaweza kufukua mchanga ambao nao umefunikwa na kichaka kilichoota juu ya kaburi na bado tukawa na matumaini ya 'kufufua' na kurudisha uhai wa marehemu? Ninachosema ni kwamba nia njema ya kumfukua marehemu itakosa maana kama suala la kuurudisha uhai litabaki kuwa la kiimani zaidi. Kwa hili la JUMUWATA, nadhani itoshee hapo mpaka mizimu yenyewe itakapomfukua marehemu kwa miujiza. Miujiza maana yake mchakato usieleweka kwa akili za kawaida. Mara nyingine kukata tamaa ni maumbile.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, January 13, 2010

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo