Recent Posts

kikombe kimoja tu cha kahawa,kisha nijiondokee
japo nimekuja kukujulisha,
kuwa kusho nakuacha
ili nisiendelee kukupamachungu zaidi
kikombe kimoja tu cha kahawa,kisha nijiondokee

nimeleta pesa kama vile yule mwanasheria alivyosema
lakini haiwezi kuwa mbadala ya maumivu nilikusababishia
wala haitachukuwa nafasi ya mpenzi wewe,najua
kikombe kimoja tu cha kahawa,kisha nijiondokee

waambie watoto kuwa nilikuja usiku uliopita
nikawabusu wakati wakiwa usingizini
nitengenezee kahawa yangu iwe tamu na moto
kama vile ulivyozoea kujilaza katika mikono yangu

japo kikombe kimoja tu cha kahawa kisha nijiondokee
kikombe kimoja tu cha kuhawa kisha nijiondokee.

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, January 16, 2010

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo