Recent Posts

vazi lako la kiafrika lanikumbusha kuhusu wewe rafiki,
u mrefu kiasi,
mwembamba kiasi,
u msheshi si kiasi,
u mawazoni raki.

siku,mwezi sijakuona rafiki,
ingawa muda ulitupa mkono rafiki,
mengi kutoka kwako nakumbuka rafiki,
u mawazoni rafiki.

zawadi nitaipata tena rafiki,
ingawa nilisusia rafiki,
kwa kuwa nilijifikiria mwenyewe rafiki,
naamini zawadi ili nitaipokea tena rafiki.

vazi lako la kiafrika nalikumbuka,
na tuk tuk kupanda,
upepo na baridi kutupuliza kama puto,
sikuchoka kuwa nawe rafiki.

Mungu akujalie pale ulipo rafiki,
naamini tutakutana tena rafiki,na zawadi kuipokea,
nami shairi nitakuimbia,dis poem nitakuimbia.
u mawazoni rafiki.

Posted by nyahbingi worrior. Tuesday, January 19, 2010

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo