Recent Posts

Naanza na ya kale.

Kale ni kitambo kidogo,wakale walifanya mambo yao kwa uhakika zaidi.Naamini ni mengi ya kale mazuri yaliyojitokeza katika wanajamii wa kale ambayo yamenzaa mema mazuri ambayo hayaeshimiwi tena katika mambo ya kisasa.

Ili kupata maendelea mazuri katika jamii inabidi jamii iheshimu Mila na Desturi na sio civilization au globalization.Sayansi hii ya kisasa inatupeleka wapi?Mbona sayansi ya kale ilikuwa bomba kichizi?

Kwa mfano,kazi ya mme na mke zilikuwa zipi katika mila na desturi fofauti tofauti?

Kwanza kulingana maandiko takatifu,Mungu alimuumba mwanaume mfalme wa kila kitu ambacho kiko karibu naye,kisha Mungu akamuumba mwanamke kutoka ubavu wa mwanaume(ubavu mmoja tu) baada ya kuona mwanaume anazidi kuboreka.

Mwanaume alikuwa na majukumu yake ya kila siku,majukumu ya kulinda familia,jukumu la kuwa msemajii mkuu katika familia.Narudia tena msemaji mkuu.Mwanaume aliwajibika kutafuta kila mema katika familia na jamii kwa jumla.

Mwanamke alikuwa na majukumu yake katika familia.Mwanamke alikuwa daktari au mlezi mkuu wa familia,mwanamke aliwajibika kumakesure familia inapata mahitaji kama vile chakula,usafi na alipaswa kujuwa ugonjwa wowote ule katika watoto.

Watoto walitengwa katika makundi mawili tofauti.Kundi lakwanza watoto wa kiume na kundi la pili watoto wa kike.Labda unaweza uliza kwanini.Watoto wa kiume walifundishwa mambo ya kiume kama vita,ujenzi,familia n.k.Watoto wa kike walikuwa karibu sana na wazazi wao wa kike na kufundishwa maswala yote ya jikoni na jinsi ya kumlea mume.

Wakati wa mikutano au ugeni.

Mikutano yote ilihudhuriwa na kusikiliza na wanaume.Wanaume ndio walikuwa na uwezo wa kutoa ushauri na kupendekeza nini kifanyike katika jamii husika au swala husika.

chakula.

wanaume waluikuwa na vyakula vyao ambavyo mwanamke haruhusiwi kula kamwe.Na ikijilikana mwanamke kala basi balaa kubwa liliweza kukumba jamii hiyo.Katika vyakula vya wanaume viligawiwa kiumri na heshima katika wanaume.

Haya ni kwa ufupi tu,lakini swali linabaki palepale,je haya mambo ya kisasa yanafaida yoyote katika jamii au familia.

Katika hali ya kisasa watoto au mama waweza kuanza kula hata kabla baba hajarudi toka kazini,i mean wanaweza kupakuwa na kuanza kula.Katika mambo ya kisasa tunaona wote(wanaume,wanawake na watoto)wanahudhuria mikutano pamoja na kuchangia mada.

Tukumbuke za kale zilisaidia kwani licha ya babu kuoa wake wengi lakini hakukuwepo na jangwa la ukimwi au utumiaji wa kondom,lakini leo hii inashangaza sana na mambo ya kisasa licha ya kondom,licha ya ndoa zenu takatifu,licha ya pete zenu za dhahabu, bado naona gharika.Gharika ambalo linazidi kumeza wengi kwasababu hatuheshimu tena mila na desturi,kwasababu katika mambo ya kisasa hakuna tofauti kati ya majukumu ya mwanaume na majukumu ya mwanamke.

Posted by nyahbingi worrior. Tuesday, February 9, 2010

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo