Recent Posts

wajukuu,vitukuu na vijikuu,hapo zamani za kale,ohhhhhhh hapana sio zama za kale zama za leo,ndio leo hii,sasa hivi napozungumza nawe,mnaponisilikiza wajukuu naongea nanyi wajukuu.

Kwa kuwa nilijiwa nikatumia neno hadithi ili mje kwa wingi na kunisikiliza nnachotaka kusema wajukuu.Sio hadithi tena bali ni ukweli wa matendo ya leo wajukuu,kwani ni heri kukutana na simba kuliko kukutana na binadamu wajukuu.

Wajukuu mnakumbuka kifo cha baba na mama nani,watoto wao leo hii wanataabika wajukuu,ndugu ambao ni binadamu walikombo kila kilichokuwa mbele yao na kwenda zao.

Wajukuu mnamkumbuka Da nani alijifunguwa na mtoto kumtia majini(chooni).

Wajukuu hadithi itaaendea wajukuu lakini kabla hamjasambaratika nawatangazia biashara yangu nzuri ya kupamba maiti.Karibuni sana.

Posted by nyahbingi worrior. Monday, August 16, 2010

2 comments

  1. emu-three anasema:
  2. Hadithi njoo, ukweli uje na uwongo usije

     
  3. bila uongo kuna hadithi kweli?

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo