Recent Posts

kwa lugha ya kwetu siwezi hata kuzungumza ila naweza kuzungumza lugha mbalimbali kama vile kisweden,kifaransa,kichina,kijerumani n.k.

Nashindwa hata kuzungumza na mkewangu palipo na umati wa watu ile wasituelewe lakini naweza kuzungumza na msweden kisweden,kifini na mfini,kifaransa na mfaransa n.k

Siwezi kutongoza kikwetu lakini naweza kutongoza au tongozwa kwa kifini,kisweden,kifaransa nk.

niliona nifahari kuhutubia kwa kifini au kiingereza lakini kumbe wengi hawakunielewa.Sasa najuwa kwanini wachina wanazungumza kichina na si kiingereza au wajerumani na kijerumani chao.

Kichaggha siwezi ila kisweden naweza,
kimakonde chanipiga chenga ila kifini usiseme,
inachekesha sana,na manadai kwa lugha yenu ina HUU?

au wengine kwasababu nimewagusa mtaishia kusema ILI NALO NENO......

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, August 19, 2010

1 Responses to lugha ya genini na kutokujuwa mimi ni nani.

  1. Yasinta Ngonyani anasema:
  2. kaka umeifanya jioni yangu iwe ya njeeema kabisa kwani mimi siwezi kisweden ila naweza kingoni... halafu unajua namsifu sana mwl. Nyerere kwa kutaka watu wote Tanzania yetu waongee Kiswahili kama Lugha ya taifa. Lakini pia nasikitika kwa vile wengi wanajifanya sasa eti mimi siwezi kuzungumza kingoni naweza kifini au kisweden...wanasahau kuwa wao ni akiana nani???kaazi kwelikweli. Ahsante kwa leo!!

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo