Baba ni jina la majukumu katika familia pamoja na majirani.
Mtoto atamtambuaje baba yake?
Je,atamtambuwa kwa kuwa mama yake alimwambia huyu ni baba yako?
au
Mtoto atamtambuwa baba yake kwa vitendo?
endapo baba anarudi nyumbani mikono tupu hata bila mfuko wa rambo mkononi inakuwa vigumu kwa mwanae kumchangamkia.
Sunday, March 20, 2011
Ulezi au utambuzi wa mzazi kama baba, upo katika sehemu mbili, baba kwa kuzaa, na baba kwa ulezi. Wengi wanabeba majukumu yote hayo kuwa ni baba kwa kuzaa na ulezi pia.
Mtoto ana wajibu wa kumtambua baba yake, kuwa ndiye aliye mzaa(kutoka mama, au kutoka kwa baba, au historia na kumbukumbu zitaonyesha). Lakini je baba huyo atakuwa baba kamili kwa kuzaa tu? Hapana lazima wajibike ili apate ile sifa kamili ya baba mzazi, na malezi pia!
Matendo ni muhumu sana kama wajibu wa mzazi(baba), sio vyema ukazaa tu na kutamba kuwa mimi nina mtoto, wakati kula au kulala hujui huyo mtoto anavipataje...labda uwe na dharura ambazo hazikwepeki!