Recent Posts

wakati mimi nawaza kupanda daladala,mwingine anawaza kupanda ndege.

wakati mimi nawaza cha kupika,kuna yule anachaguwa cha kula au kupika.

wakati mimi nawaza jinsi ya kupata maji ya kunywa,kuna yule anachaguwa bia ya kunywa.

Wakati mimi nawaza kununuwa neti ya mmbu,kuna yule anachaguwa dawa ya mmbu.

wakati mimi natafuta nauli,kuna yule kibubu chake kimejaa chenji.

wakati mimi nawaza jinsi gani ya kujikinga na ukimwi,kuna yule condom kwake ni kichefuchefu.

wakati mimi nawaza nguo ya kuvaa,kuna yule anavaa suti.

wakati mimi na hubiri kuna yule anazini.

wakati mimi nasoma tangazo la uvutaji wa sigara,kuna yule anavuta sigara.

wakati mimi nawaza pindi Yesu atarudi,kuna yule kamkumbatia shetani.

wakati mimi nawaza ntapata wapi ngono,kuna yule anawawili kitandani.

wakati mimi nawaza kwenda Kariakoo,kuna yule anawaza kwenda sweden.

wakati mimi nawaza kuna na familia,kuna yule anataka talaka.

wakati mimi nawaza kwenda haja kubwa,kuna yule anawaza kwenda hajaa ndogo.

wakati mimi nawaza kuacha pombe,kuna yule anapenda pombe.

wakati mimi na waza siku ya kufa,kuna yule anasherehekea siku ya kuzaliwa.

wakati mimi nawaza kupata ujauzito,kuna yule anatoa mimba.

wakati mimi nawaza kuoa binti wa kiafrika,kuna yule kaolewa na mgeni.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, May 1, 2011

1 Responses to nawaza.

 1. SIMON KITURURU anasema:
 2. Kwa kifupi,..
  ... KUNA siye na WALE
  ...MIMI na YULE,...
  .....WEWE na WENGINE,...
  ... na mwisho wa siku yako ni yako.
  Si unakumbuka ulizaliwa peke yako na utakufa kivyako peke yako kwa hiyo labda kufikiria ya wengine ni LUXURY tu za MAISHA?:-(

   

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo