Recent Posts

Sikubahatika kupata kiti ndani ya daladala.Nilikuwa natokea posta kwenda Mwenge jana mida ya saa saba,nane mchana.

Mbele yangu kuna dada kaketi,gafla katoa simu yake ya kiganjani kaanza kutuma sms.Dada huyu ni mtu mzima kwa kumwangalia lakini nilishtuka na sms ambazo niliweza kuzisoma pasipo yeye kujuwa napiga chabo.Nilivutiwa sana na umahari wa dada yule katika kutunga na kutuma sms.

Moja kati ya sms ilisema hivi,

Honey i do love you so much,nakupenda mpenzi wangu,naomba unitumie elfo 70 kwa M-Pesa.

Gafla akajibiwa..

Dear nitakutumia muda si mrefu.

Baada ya muda kidogo,yule binti akampigai shosti wake na kumwambia leo tunatoka jioni,Mr X anatuma mshiko.

Akafika maeneo ya moroco akashuka.Mimi niliendelea na safari yangu lakini sikupata kupiga chabo tena.

Jamani STAREHE GHARAMA.

Posted by nyahbingi worrior. Friday, June 24, 2011

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo