Recent Posts

Maisha ukishayapatia bwana,vile vyote ulivokuwa unavifanya awali waviona kama havina maana lakini maisha yakikuyumbisha tena kidogo unakimbilia vile vya awali na kuviona vinafaa sana.

Kuna yule kabla maisha hajayapatia alikuwa mpenda michezo sana lakini maisha kayapatia michezo aiona haifai tena.

Kuna yule kabla maisha hajayapatia alikuwa hakose kukaa vijiweni na kupiga stori lakini maisha kayapatia hata vijiweni haonekani tena.

Kuna yule kabla maisha hajayapatia alikuwa hakose katika nyumba ya ibada lakini baada ya kuyapatia maisha na ibada kaona haifai tena.

Kuna yule alikuwa msomaji mzuri wa blogu na na mwandishi mzuri wa blogu lakini,na blogu kaona kupoteza muda.

Kuna yule kabla hajayapatia masha alikuwa na mpenzi mwenye rangi ya Nguvu kuliko zote,lakini baada yakuyapatia maisha ile rangi yenye Nguvu aiona kama kichefuchefu.

Maisha ukiyapatia bwana,hata mwendo unabadilika.

Je,umewezaje kuyapatia maisha?

Kuna yule akikipata akipendacho basi kwake maisha ashayapatia.

Posted by nyahbingi worrior. Monday, August 8, 2011

1 Responses to Maisha ukiyapatia.

  1. SIMON KITURURU anasema:
  2. Swali ni:

    Je,unawezaje kuyapatia maisha?

    Mie nahisi kunakujidanganya katika BINADAMU kama BINADAMU atafikia kujiamini anapatia!:-(

    Na kuna wabadilishao staili ya maisha kwa kuwa HAWAJAPATIA aisee na kutokupatia+UMRI unaweza kujikuta hali mbaya kuliko zamani!:-(

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo