Recent Posts

Sio wote wenye uwezo wa kulala ingawa tunaamini wote tunalala.

Swali.........

Giza maana yake wakati wa kulala umefika?

Giza maanake wakati wa tendo la ndoa umewadia?

Hivi.....

Kwanini wengi wetu hupenda kujamiana wakati wa KIZA kinene?

Turudi kwenye MADA.

Naamini wengi wetu hatulali ila tunakesha kwa kufumba macho na kusingizia tumelala.Naamini wale ndugu zetu waishio UGENINI hulala usingizi fofofo na kuota ndoto nzuri za nyumbani ingawa hawapendi kurudi nyumbani kwani nyumbani kwao kumekuwa UGENINI licha ya wao kuzoea UGENINI.

Hivi...

Kwanini NANI hatakaki kurudi NYUMBANI?

Yule asinziae UGENINI hupata muda mwafaka wa kutafakari rafikiye wa UGENINI anamfikiriaje pia apumzikaye UGENINI hupumzika na wenyeji kiasi ambacho humfanya MGENI kuamini yuko NYUMBANI.Mwenyeji kwa Mgeni kwake humshika ngozi yake na kushangaa lakini cha kustaajabika MGENI haelewi kwasababu naye ajiona ni mwenyeji.

Ifikapo siku ya kuzaliwa UGENINI,MGENI huimbiwa na WENYEJI kiasi ambacho MGENI kujiona MWENYEJI kamkaribisha MGENI MWENYEJI.

swali....

Kwa mtazamo wako,je umewahi kulala?kusinzia?au kupumzika?

Posted by nyahbingi worrior. Monday, October 10, 2011

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo