Recent Posts

Jamani tuache kumchosha Mungu kwasababu Mungu anakazi nyingi sana za kufanya.Tumekuwa na tabia ambayo haifai katika jamii na naamini haimpendezi Mwenyezi Mungu.Kwasababu kila jambo linalomkuta mwanadamu humlaumu Mungu.Kwa mfano,mtu amekufa,utasikia waombolezaji wakidai kazi ya Mungu,sasa mimi naomba kuuliza,kuna kiumbe ambacho hakifi?Kwa swala la kifo wala tusimtaje Mungu bali tukubali hali halisi.

Mtu kafeli,utasikia Mungu hakupenda,yani mwanafunzi hasomi anafeli,unasema Mungu hakupenda?
Mtu kaacha na mumewe/mkewe utasikia Mungu hakupenda?
Mtu mimba imeharibika tumboni utasikia Mungu hakupenda?
Mtu kaachwa na mpenzi wake utasikia Mungu alikuwa ananiepushia balaa?
Mtu kapata ajali utasikia wakimlaumu Mungu/

Jamani nawasii mengi tujilaumu sisi wenyewe,mwanafunzi kapata ujauzito utasikia ilishapangwa na Mungu.

Mhhhhhhh jamani.

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, June 9, 2012

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo