Recent Posts

Nacheka nikikumbuka wasemavyo mke mwema hutoka mbinguni,
wao wajuo mengu hunena na kusema mke mbaya hutoka mbugani,
mume hupaswa kutafuta ushauri kwa waume wenzake,
mke naye hupaswa kutafuta ushauri kwa wake wenzake,
mume hapaswi kuomba ushauri kwa mkewe.

Maelewano mazuri ni pale pasipokuwa na maelewano kati ya mume na mke.Kwasababu gani nasehema hivi.Mke akimuelewa mume,maswali yasiyo ya sekondari huibuka na huitaji majibu ya msingi.

Mila yangu mimi,nakumbuka jinsi gani bibi alikuwa na kibanda chake na babu na kibanda chake pia.Babu yangu aliamuwa alichoamuwa kwa sababu yeye ni SIMBA wa nyumba.Nakumbuka jinsi gani bibi alikuwa anaweka chakula mlangoni kwa babu kwani aliku na siku maalumu ya kuingia katika nyumba ya babu.

Bibi na babu walikuwa wanakutana mashambani licha ya kuwa katika boma moja.

Sasa angalia licha ya baba na bibi kuishi ivo miaka nenda rudi sikuwahi kusikia neno UKIMWI.Angalia leo,licha ya mume na mke kulala kitanda kimoja UKIMWI bado watawala na kuwa na kinga chini ya MTO kila usiku.

Kwanini mume atumie kinga kwa mkewe?jibu rahisi kabisa(MAELEWANO)

Unaposoma haya makala tafadhali rejea na shairi la DIS BLOG.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, September 20, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo