Recent Posts

Mwanzo ulikuwa mtamu,
sikujuwa kama nitapiga mtama,
nanyanyuka kinamna,
naandika kwa maana,
natafakari kinamna.

Hapo zamani,
zama zile,
enzi za mazee wetu,
enzi za mvi na busara za kukubalika na watu wetu,
enzi za jando ni nini,
enzi za tohara ni nini.

amini usiamnini,
maisha ni kama nini,
mapenzi ni kama nini,
si tamu kama nini,lakini sijui ni nini.

ujasiri ni lazma,
mkongojo si lazma,
nakaza gidamu kwani ni lazma,
siwezi kuwa mtumwa kwa lazma.
mwanga niuone lazma.

kwa mlio tangulia,wengi hawakuamini,
hata mimi sikuamini,kwa kuaminiana mmeamini,
ni kama kitendawili,watatu,wanne wawili kukiteguwa,
kuku katagia mwibani,wala sio ubani,
au msibani?

Posted by nyahbingi worrior. Monday, October 5, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo