Recent Posts

piga ua talaka utanipa,
nimechoshwa na vibwanga,
nimechoshwa na ndao hii takatifu,
talaka utanipa tu.

sijui niliwaza nini nilipokubali uwe mke wangu,
sijui niliwaza nini nilipokubali uwe mme wangu,
umenifika kooni,nasubiri tapika,
talaka utanipa tu.

mwanamke gani weye,suruali isipite mbele yako?,
mwanaume gani weye,sketi isipite mbele yako,?
mwanamke huchoki?
mwanaume huchoki?
au kwa sababu si sabani itaisha?
talaka utanipa tu.

na pete chukuwa,
sikupendi mwanamke wewe,
sikupendi mwanaume wewe,
talaka utanipa.

watoto nakuachia,
kwanza wote wakike,nani anataka malaya?
kwanza wote wakiume,nani anataka malaya?
talaka utanipa tu.

kwetu narudi,
talaka utanipa tu.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, December 9, 2009

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo