Recent Posts

Sio kama leo,
mwanablogu kuhabarisha kuhusu "happy birthday",
yanini wakati watu wanataka kuhabarika,
enzi zetu kaka,dada,wajukuu,
we were bloggers.

miaka ya 2006,2007,
tuliumiza vichwa bwana,
kutafuta habari ya kuhabarisha,
sio kama leo bwana,
blog zimesheni picha za kujidai,
enzi zetu wajukuu
we were bloggers.

nuru ilionekana,
jumuiya kuanzishwa,
jumuwata wajukuu,
sip kamaleo wajukuu,
hata jumuiya jumuwata hajui nini huku mwajigamba eti wanablogu,
wajukuu enzi zetu,
we were bloggers.

leo kuna makundi makundi,
sote bloggers lakini makundi makundi,
habari zao za makundi makundi,
makundi?
enzi zetu wajukuu,
we were bloggers.

na wawakilishi kuchaguliwa,pasipo kujuwa msimamizi wa uchaguzi,
kura kuhesabiwa,kukosa nilikosa,
na jumuwata kuzikwa,
kichwa tu chabaki,
enzi zetu wajukuu,
we were bloggers.

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, January 7, 2010

1 Responses to WE WERE BLOGGERS.

  1. Well said Man
    Nuff Respect Mankind. I hope tutaliangalia hili kwa JICHO LA NDANI

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo