Nilitegemea blogu nyingi za ndugu zetu watanzania waishio ughaibuni kublogu kuhusu ughaibuni lakini kumbe sio bado wanakumbuka nyumbani.Duh!!
Wednesday, February 3, 2010
Nilitegemea blogu nyingi za ndugu zetu watanzania waishio ughaibuni kublogu kuhusu ughaibuni lakini kumbe sio bado wanakumbuka nyumbani.Duh!!
Nyabhingi: Home is where your heart is. Kwa hiyo wanaweza kuwa Dar lakini wanawaza matobholwa kule Sangamwalugesha :-(
Ninaye yangu yuko USA yeye anadai kuwa akifa hata iweje ni lazima arudishwe aje azikwe pembeni na alikozikwa mama yake. Na akisikia nduguye yeyote ana shughuli ya arusi atapanda pipa na kuja huku kula mapochopocho ya nyumnani.
hivo usishangae sana kwa hilo
Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!
Chacha,wengi utakuta wanazungumza mapungufu ya Tanzania na mazuri kusahau.
Nami nafurahi kuona jinsi gani wanakumbuka nyumbani.
amani.
nyumbani ni nyumbani
kuna mutu aliwahi kusema 'be the change you want to see'. Kama wanaongea mapungufu bila kuangalia ni kwa jinsi gani wenyewe wameshiriki kuyatengeneza ama kuyafanya yaendelee hapo ndo kuna tatizo....:-(
Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!
Ni kama wewe tu Lui, Uko Kinondoni lakini roho yako yooote iko migombani Uchagani. Si unaona mwenyewe unavyoliongelea Jembe japo unalikwepa kiaina?
Da Mija,silikwepi jembe.Unataka nijichanganye hapa.