Recent Posts

Blogu zazidi kuwa nyingi kama wasanii,
waimbao tungo za mapenzi,wakati wanajamii wananjaa ya maendeleo,
wafunguwa blogu kutafuta sifa?
au,
wafunguliwa blogu na kuandikiwa?

blogu nyingi,hakuna umoja(jumuwata)
wanablogu wakutana,kuishia kupiga picha,
vichwa vyahabari vyahuzunisha,
walioko ughaibuni waandika ya nyumbani,
kwani kwao ugenini ndio nyumbani.

blogu nyingi
maandishimi mengi,
hadithi nyingi,
happybirth day nyingi,
kusalimiana kwingi
mabadiliko ZERO.

wengine tukubali kuwa wasomaji,
habari moja,
blogu 100.

blogu moja yahojiwa miaka 100
bado tuko miaka 100.

Posted by nyahbingi worrior. Friday, May 28, 2010

4 comments

  1. Fadhy Mtanga anasema:
  2. Changamoto ya aina yake.

     
  3. Yasinta Ngonyani anasema:
  4. Kaka kuna mabadiliko ya aina yake!!

     
  5. labda, swali, wafungua blogu kkulalamikia blogu??

    blogu nyingi chagua moja uipendayo tembelea hiyo kwani ndiyo uipendayo, ussiwe na hofu Umoja waweza kuuleta wewe na ndiomaana upo

    wadhani hautuna umoja?? mbona twatembeleana au umoja upi si lazima tuanze na huu, si kutembelea blogu yako ni umoja wa kukutambua??


    sorry najiuliza tu na mimi sio mtunzi wa vina

     
  6. Christian Bwaya anasema:
  7. Nakusalimu rasta

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo