Recent Posts

ukinusa harufu tu ya pilau utakimbilia kula lakini baada ya mikono miwili wakinai.Jiulize blogu yako ni aina ya pilau?

Barabara ya Mtwara kula Dar kuna takribani kilomita kama 65 ambazo dereva atatumia masaa 4 kufika mto Rufiji.Jana nilipata madhari mazuri nilipowaona VIboko katika mto Rufiji karibu kabisa na daraja.

Tukiwa katika kipande kibaya ndani ya kilomita 65,mabasi mengi yalikwama kutokana na mvua na hali halisi ya kipande hicho cha kilomita 65.Nilishuka katika basi na kwenda kutoa mchango ni nini kifanyike ili basi yaliyo kwama yaweze kuyapisha mengine ambayo hayajakwama.Nilishangaa kuona abiria hawataki kuteremeka na kutoa nguvu wakati wa kusukuma magari,inashangaza kuona binti au kijana kajipulizia sijui nini then hataki kuchafuka.Nikajiuliza hivi hawa vijana wa kileo wanatahiria kwa staili gani?na kwanini wanapiga vita msichana kuto tahiriwa?

vijana ambao wanategemewa,vijana nguvu ya leo wanaishi kama TAUSI?

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, May 23, 2010

6 comments

  1. Yasinta Ngonyani anasema:
  2. naona umerudi na upo nasi pia karibu sana katika familia hii. "ukinusa harufu tu ya pilau utakimbilia kula lakini baada ya mikono miwili wakinai.Jiulize blogu yako ni aina ya pilau?" nimependa sentensi hii

     
  3. mdoti Com-kom anasema:
  4. si wote hukinaiwa na pilau ndugu! tazama wengine hawatakuelewa japo ni vizuri kuuliza je blogu yako ni kama pilau? kwa namna yoyote unayoweza kutafsiri.

     
  5. Duh!! Niingie kwenye suala la safari za kuelekea KUSINI.
    Nilipokuwa mwanafunzi wa Ndanda Sec, kuna siku tulilazimika kushuka na kusukuma gari inayowaka. Yaani maeneo ya Nanjilinji yalikuwa ni "mlalo" zaidi ya "mpito". Ilikuwa ni safari ya kujipanga. Ujue utaondoka na kulala rufiji huku ukijua kabisa kuwa "dina" yako ni Pweza (well, kulikuwa na chaguzi nyingi ila nilipenda Pweza na chachandu ya kunyunyizwa kwa kijiti na katani) na kisha mkiamka hapo mnajiandaa kwa "juu-chini" ya barabara mpaka mkifika
    Hii ilikuwa kabla ya daraja na matengenezo ya barabara.
    Nasikitika kusikia kuwa mambo yakingali vilevile.
    Kaka. Lililo kuu na muhimu ni kuwa umerejea na umerejea ukiwa imara na mwenye fikra pevu zaidi
    Blessings

     
  6. chib anasema:
  7. Mkuu pole na maswahiba hayo. Yaani km 65 tu masaa 4!!!! Sijawahi kupita barabara hiyo achilia mbali kufika Mtwara.

     
  8. Mija Shija Sayi anasema:
  9. Mzee wa mawaidha afadhali umerudi uturudishe kundini. Karibu sana.

     
  10. nawashukuru nyote kwa maoni yenu.tuzidi kuwa pamoja ingawa huko mliko si nyumbani.

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo