Recent Posts

hakuna anayetaka kufa,
wale anayependa kifo,
wapo wanaotaka na wanapenda kwenda mbinguni,
wapo wanaosali ili Mungu azirefushe ziku zao hapa duniani,
najiuliza watafikaje huko?Pasipo kufa?
au kama wote tukisali tusife na nani atakufa?
hawa ni wale wanaoitaji mwanga wa tochi mchana peupe.

waweza kukibemba kiumbe miezi 9,
waweza kubeba kifo ndani ya mienzi 9,
hawanaatia lakini wachukuliwa ndani ya miezi 9,
je wewe waweza kubeba mzigo kifo kwa miezi 9?

twatakiana mema mengi,
heri ya pasaka,krismasi,happybirthday,kuzaliwa,
twatakiana pia,
sikunjema,kazi njema,usiku mwema,uguwa pole
bado sijapata sikia,
nikutakia kifo chema au,
heri ya kifo chako au changu,
kwanini?
kwani hujui kifo ni siku ya sikuku kama sikuku zingine?
tafakari..,

mwenye kuzaliwa apewa cheti angali hai,
mwenye kipaimara apewa cheti analia hai,
mwenye ubatizo apewa cheti angali hai,
mwenye kuoa/kuolewa wapewa vyeti wangali hai,
kwanini nisipewe cheti cha kifo angali hai?


Mila na desturi ziliwafanya babu zetu kushinda hofu ya kifo,
leo vijana na utandawazi hawataki kusikia habari NZURI ya KIFO,
wazazi wengi wa leo hawewezi kuwaelezea watoto wao Utamu wa Kifo.

Kama mshale wa saa,
nami kifo chanikaribia,
yanipasa niwe shujaa,
kuyashinda mauti.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, June 6, 2010

3 comments

 1. Fadhy Mtanga anasema:
 2. Umenifikirisha sana

   
 3. Kaka Fadhy,tukubali kifo kama tunavokubali sikukuzingine.Mimi nadhani hata KIFO ni sikuku kama siku zingene,sema tu bado tuko gizani.

   
 4. ishu ni kupewa vyeti vyetu vya kifo tukingali hai, vinginevyo tuwe tunawapatia watoto vyeti vya kuzaliwa kabla hawajazaliwa pia,

  suala la kifo nimewahi kuliongelea saana ila jamiihaitaki. inashangaza, kulia lia misibani wakati mwingine

   

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo