Recent Posts

Unajuwa bwana,wakati mwingine napenda sana kutumia lugha ya kulee kwa kina nani....

Leo nimepata taswira za nyuso za watu wanaotoka makwao kwenda kutafuta mkate maeneo tofauti tofauti ya jiji la mzizima.

Ni alfajiri na mapema,niko kituoni bima tabata,nadandia basi la kariakoo au posta,nashuka rozana buguruni.Ndani ya basi nyuso za abiri ni tofauti,hakuna hata nyuso moja inayo tabasamu,wanafunzi nao wako kimya.

Cha kushanganza.......

Ndani ya basi hakuna hata abiria mmoja kanunuwa gazeti,suka naye kaweka ule wimbo wa nani vile...unakwenda hivi...mflame wa amani,mfalme wa amani uinuliwe,wewe ni mwema,wewe ni mwema bwana..........hapa midomo ya abiria nayo inaaimba kwa kuwa kila moja wetu anajuwa kwanini huo wimbo ummemgusa.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, March 16, 2011

0 comments

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo