Recent PostsHii ndio NEMBO ya JUMUWATA(Jumuiya ya wanablogu Tanzania).Jumuwata ni chama cha wanablogu wa Tanzania.Chama hiki kinaongozwa na Ramadhani Msangi,Simon Kitururu na Da Mija Shija.Nia kuu ya JUMUWATA ni kusaidia watanzania waweze kufaidika na mabadiliko ya teknolojia.


Viongozi wote watatu wanablogu zao na zinafanya vizuri sana katika dunia ya BLOGU lakini kurasa ya JUMUWATA www.blogutanzania.com imetupiliwa mbali.Naomba nieleweke hapa,siko hapa kumlaumu yeyote yule,siko hapa kumsifia yeyote yule na SIKO TIYARI KUONA JUMUWATA INAFUKIWA,NITAPIGANA MPAKA TONE LA MWISHO,nitahakikisha JUMUWATA inasimama,inafufuka TENA.(Read my lips)


Kwa uongozi uliopo,kama mmeshindwa tafandali ninaomba mkabidhi kurasa ya www.blogutanzania.blogspot.com ili niifanyie kazi.


Funguwa kurasa ya BLOGU TANZANIA ujione,inasikitisha.Nimekuwa napiga kelele naonekana kama mwendawazi,sasa nauvaa uwendawazimu,nitahakikisha JUMUWATA inasimama.


Huu ndio mwanzo.


Uwezo tunao,Nia tunayo na sababu tunazo.


Luiham W.Ringo

nyahbingiworriors.bloguspot.com

Posted by nyahbingi worrior. Monday, September 26, 2011

2 comments

  1. SIMON KITURURU anasema:
  2. Mie nakusikia Rasta na nakusikia tokea mwanzo!:-(

     
  3. Kama kweli Simon umenisikia tokea mwanzo ungelifinya kitu lakini naona bado hujanisikia.

     

Post a Comment

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo