Recent Posts

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, March 30, 2011 0 comments

licha ya ugumu au urahisi wa maisha bado sote tunapata baraka za Mungu za mvua. jaribu kuchambuwa hii sentensi.. we all share the sun but we cant share homes. kuna wale kati yetu wanajiona wao wanafaa dhidi ya wengine,kuna wale ambao wakifika kanisani,msibani wanapenda sana uwepo wao utambulike. Kuna wale ambao baada ya kufanya tendo la ndoa hawapendi hata rafiki wa karibu ajue,pia kuna wale ambao hawapendi kuanika chupi zao hadharani. Kuna wale kati yetu wanapenda kunukia vizuri katika kundi la watu na kuna wale kati yetu hawapendi sindano. Kuna wale kati yetu wanatamani hadi leo hii wangekuwa na ubikra,pia kuna wale kati yetu hawapendi kutunza ubikra wao. kuna wale kati yetu hawezi kumfikisha mwanamke kwao kijijini na kuna wale kati yetu huwafikisha wanawake kijijini na kuwapitiliza. kuna wale kati yetu.......

Posted by nyahbingi worrior. Tuesday, March 29, 2011 1 comments

mambo ndio hayo,habari ndio hiyo,vikombe vinazidi kushamiri,siwezi pinga au kukubali ngoja nisubiri mwisho wake. Mimi naamini sana katika miti shamba,napenda kutumia dawa za kiasili lakini dawa ya kiasili inatolowe kama da wa ya asili pasipo kushirikisha swala zima la dini. Mimi siamini kama ni mwisho wa dunia kwa haya matukio kutokea.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Kina mama oyeeeeeeeeeeeee.

wasanii wengi ambao walipewa tuzo zao,wengi wao walidedicate tuzo hizo kwa mama zao.

Kina baba hawakuchangia hata kidogo?

Mimi sio mpenzi wa nyimbo za bongofleva kwa hiyo katika hili siwezi andika sana,lakini naumiza kichwa katika haya mawili..

Mpoki kaibuka mshindi dhidi ya Mrisho?
Hardman kaibuka mshindi dhidi ya Jhikoman?

Bado naumiza kichwa?

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, March 27, 2011 0 comments

Kama mtu amefiwa au kagongwa na gari,au kalazwa,kuna neno moja tu la kusema nalo ni Pole.Hii tabia yakusema ni kazi ya shetani kwakuwa flani kafa haifai,Mungu ndiye anayetoa na vilevile ndiye anayetwaa sasa huyu shetani anatokeo wapi?

Umeambiwa Nyahbingi worriors kafa,sema pole,haya mambo ya kusema ooohhhh my god this cant be,nilikuwa naye jana,namdai,ananidai yaishe.

au Mzee wa mawazoni unasemaje?

Posted by nyahbingi worrior. Thursday, March 24, 2011 2 comments

Nyahbingi Worriors,inawapa pole kwa msiba uliotokea kwa familia ya mwanablogu Da Yasitha wa ://ruhuwiko.blogspot.com/.

Sellasi I.

Posted by nyahbingi worrior. 1 comments

That until the philosophy which holds one race superior and another inferior is finally and permanently discredited and abandoned: That until there are no longer first-class and second class citizens of any nation; That until the color of a man's skin is of no more significance than the color of his eyes; That until the basic human rights are equally guaranteed to all without regard to race; That until that day, the dream of lasting peace and world citizenship and the rule of international morality will remain but a fleeting illusion, to be pursued but never attained; And until the ignoble and unhappy regimes that hold our brothers in Angola, in Mozambique and in South Africa in subhuman bondage have been toppled and destroyed; Until bigotry and prejudice and malicious and inhuman self-interest have been replaced by understanding and tolerance and good-will; Until all Africans stand and speak as free beings, equal in the eyes of all men, as they are in the eyes of Heaven; Until that day, the African continent will not know peace. We Africans will fight, if necessary, and we know that we shall win, as we are confident in the victory of good over evil.

Posted by nyahbingi worrior. Tuesday, March 22, 2011 0 comments

unajuwa bwana lugha ya kule kwa kina nani inavutia sana ndio maana wakati mwingine kama huu napenda kutumia lugha yao.

More techings,mafundisho zaidi.

Vijana wanakosa maadili kwa kuwa hakuna more techings,
vijana wanatesaka kwa kuwa hakuna more techings,
Hekima ndani yetu imepotea kwa kuwa hakuna more techings,
binadamu wanapigana kwa kuwa hakuna more techings,
misri,tunisia,libya,sudan vita tupu kwa kuwa no more techings.

kwa hiyo....

we want the youth to learn so more,RASTAFARIAN TEACHINGS.

Posted by nyahbingi worrior. Monday, March 21, 2011 0 comments

Baada ya kubeba mimba au ujauzito,mtoto anazaliwa.Baada ya muda mama atamwambia mtoto kuwa huyu ndiye baba yako na punde mtoto ataanza kumwita baba au dad kwa lugha ya kule kwa kina nani.

Unaushaidi gani kuwa huyo aliye kwambia ni baba yako?

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Baba ni jina la majukumu katika familia pamoja na majirani.

Mtoto atamtambuaje baba yake?

Je,atamtambuwa kwa kuwa mama yake alimwambia huyu ni baba yako?

au

Mtoto atamtambuwa baba yake kwa vitendo?

endapo baba anarudi nyumbani mikono tupu hata bila mfuko wa rambo mkononi inakuwa vigumu kwa mwanae kumchangamkia.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, March 20, 2011 1 comments











Posted by nyahbingi worrior. Saturday, March 19, 2011 3 comments
Posted by nyahbingi worrior. 2 comments

KIchwa cha nyumba ni MWANAUME?

Posted by nyahbingi worrior. Friday, March 18, 2011 3 comments

Kizazi cha leo na kijacho hakitapata wakati wa hadithi kama enzi zangu.Nakumbuka hadithi za bibi,nakumbuka moshi wa jikoni huku bibi akitusimulia hadithi za maadili.

Swali....

Hivi kichen party ina maadili yoyote yale?

Nukuu katika kitabu chako........

Mwanamke wa leo hapendwi kwa kukata kiono bali kwa hekima na maadili.

watoto wa leo wanahadithiwa hadithi za kukata viono tu na ndio chanzo cha kutokuwa na maadili katika jamii.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Kuna sanaa nyingi sana,kuna aina nyingi ya sanaa,kuna sanaa ya upigaji ngoma,kuimba,maigizo,ngonjera,kwaya n.k.

Wakati ule,
ule wakati wa wazee wetu,wazee wetu walienzi sanaa kwa kuikuza na kuiheshimu sio kama leo apambo sanaa ni tiketi ya kwenda ugenini.

Sanaa ya msanii wa kiafrika aishiye Afrika na kwa ajili ya Mwafrika aishiye Afrika.Ngoma ya Mwafrika ni mahususi kwa mwafrika nasio mgeni atokaye ugenini,ukimpigia mgeni ngoma ya mwafrika haelewi,anakushangaa,ngoma ya mwafrika ibaki kwa waafrika waishio afrika.

Je!umewahi kuona mgeni akitupigia ngoma zao katika bara la Afrika?

Sanaa isiwe tiketi ya kwenda kudhalilisha utamaduni wetu ugenini.

Kumbuka..

kila ngoma ya mwafrika kutoka makabila tofauti ina miko,mizimu nk,tunapopiga ngoma zetu huwa tunaitukuza mizimu,mizimu hii hutubariki kama kwa kupata mazoa mengi au mvua au kizazi chenye maadili na nguvu.

Je,kizazi cha leo kina maadili?

jibu unalo.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Unaogopa?

Leo nimepita kuuliza bei ya jeneza maeneo ya Manzese,majeneza yanapendeza sana,rangi na urembo ulio tiwa ndani ya majeneza hayo yavutia mpaka unatamani kujaribu kuingia ndani ya jeneza.

Jeneza ni bidhaa kama bidhaa ingine yoyote ile na kila mmoja wetu aruhusa ya kwenda kuangali,kuchaguwa na kuulizia bei ili ukiondoka ujuwe bei zote za jeneza.

Kuna majeneza aina tofauti tofauti.Kuna Jeneza la watu wenye fedha,wa kati na walala hoi.

Baada ya kufurahisha moyo wangu kwa kuangalia aina tofauti ya majeneza niliamuwa kwenda Mortuary.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Kuna wale wanao ishi na kuna wale wanaosindikaza wale wanaoishi.
Kuna wale wanao lala na kuna wale wanaopumzika.

Umewahi kujiuliza umuhimu wa kuwepo hapa duniani?

Ni vitu gani ambavyo vinamfanya binadamu awepo hai?

Je kwa maisha ninayoishi mimi au wewe unaona umuhimu wowote wa kuwepo hai?

Kuna wale wapendao kuwepo hai ili kutimiza mambo flani katika maisha yao na kuna wale ambao wapo hai kwasababu tu Mungu bado hajaamuwa mambo yake.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments


Posted by nyahbingi worrior. Thursday, March 17, 2011 3 comments


http://ruhuwiko.blogspot.com/

Wakati nikiwa Mtwara nilikuwa nakula sana chakula cha aina hii.Samaki Mtwara wana bei sana,hao dagaa hapo labda wanaweza kuwa wamenunuliwa kwa kiasi cha shilingi 5000,kwani kila fungu la dagaa ni 500.

Licha ya hali ya maisha ya Mtwara kuwa magumu lakini mpake leo hii,napamiss sana Mtwara.

Posted by nyahbingi worrior. Wednesday, March 16, 2011 2 comments



Hii ni moja ya kazi ya Da mija,naamini Da Mija anavipaji vingi kwani mara kwa mara hupachika kazi za mikono yake hapa http://damija.blogspot.com/ .Hongera sana Dada.
Naamini wengi wetu ambao tuko huko ni mara moja au kwa nadra sana kula au kutengeneza vitu kama hivi.Naamini wengi tunaweza kutengeneza mambo kama haya ila vikwazo vingi.
baadhi ya vikwazo ni....
Gharama za maisha zimepanda.
Ukubwa wa familia.
umeme ndio usiseme.
mkaa bei kama ya gari.
Tunachoweza kufanya wa huku,tunakula kwa macho,si muda mrefu vitumbua navyo tutakuwa tunakula kwa macho.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Unajuwa bwana,wakati mwingine napenda sana kutumia lugha ya kulee kwa kina nani....

Leo nimepata taswira za nyuso za watu wanaotoka makwao kwenda kutafuta mkate maeneo tofauti tofauti ya jiji la mzizima.

Ni alfajiri na mapema,niko kituoni bima tabata,nadandia basi la kariakoo au posta,nashuka rozana buguruni.Ndani ya basi nyuso za abiri ni tofauti,hakuna hata nyuso moja inayo tabasamu,wanafunzi nao wako kimya.

Cha kushanganza.......

Ndani ya basi hakuna hata abiria mmoja kanunuwa gazeti,suka naye kaweka ule wimbo wa nani vile...unakwenda hivi...mflame wa amani,mfalme wa amani uinuliwe,wewe ni mwema,wewe ni mwema bwana..........hapa midomo ya abiria nayo inaaimba kwa kuwa kila moja wetu anajuwa kwanini huo wimbo ummemgusa.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Kama umepata nafasi ya kuoa au kuolewa na wakati unaowa au unaolewa hukuwa bikra mshukuru Mungu wako.

Swali?

Kwanini dada zetu wanashindwa kujizui na kupoteza ubikra wao kabla hawajaolewa?

Mimi ningependa nioe tunda ambalo bado halijamegwa kwani tunda ambalo limemegwamegwa si tunda tena bali ni uchafu kwani kila aliyemega kamega na kubakiza madhara yake ndani ya tunda hilo.

Mwali mweee.

Posted by nyahbingi worrior. 2 comments

Kwa ile lugha ya kina nani wanasema wether forcast(kama nimekosea nani kwakuwa uko kwa nani naomba urekembishe).

Naamini hata habari ya hali ya hewa yaweza kuwa ya utumbo lakini mimi na wewe tukabaki kukuna vichwa.

Unawaza ya kesho wakati huwezi hata kurefusha urefu wa nywele zako.Tulia,BREAKING NEWS pia yeweza kuwa ya utumbo pasipo mimi na wewe kujuwa kama kweli ni breaking news(kwa lugha ya kina nani ambao wanakula kwa kutumia umma mwaweza kutafsiri breaking news ni nini).

Habari iliyofika humu ndani ya blogu yaweza kuwa ya utumbo pasipo kujuwa kwanini ni ya utumbo na mwambdishi kapachika.

Mhariri wa blogu hii aweza hariri habari angali akijuwa ni utumbo wa habari.

Breaking news,kwakiswahili je?

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

uozo uliomo ndani ya dili.Dili likikamilika jiulize kwanini limekamilika,dili laweza kuwa tamu pasipo kujuwa uozo wa dili hilo.

Mkeo au mmeo aweza kukuletea dili la uwozo lakini kwakuwa wewe wamwimini sana mkeo au mmeo unapuuzia.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Miguu ya habari sio tena kichwa cha habari.

Naamini kuna habari ambazo zinastahili kupewa kuwa vichwa vya habari na vile vile kuna habari zinaweza kupewa miguu au utumbo wa habari.

Posted by nyahbingi worrior. Sunday, March 13, 2011 1 comments

Kuna watu kati yetu au kuna bin adamu kati yetu wanajiona wao wanafaa zaidi ya wengine,pia kuna watu au bin adam wao wanapenda wapewe special interest zaidi ya wengine.

Nabii Afande Sele wa Morogoro aliwahi kuuliza na bado anauliza,kuna tofauti gani kati ya wale wanaoishi masaki na manzese?kwani wote hawa wawili wakifa miili yao haiozi?

Kuna watu wanadhani ya kwamba Mungu atawapa special interest kipindi wanakufa.Miili yetu ni vumbi,tutarudi mavumbini,haijalishi wewe au mimi uko uegenini,umeolewa,unawatoto,una mali n.k.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Inasemekana........

Mtoto akiwa karibu sana na baba yake huwa anafaulu katika maisha,lakini mtoto akiwa karibu sana na mama yake huwa total failure katika maisha.

Je,kuna ukweli katika haya?

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, March 12, 2011 0 comments

Wajuwa?

Posted by nyahbingi worrior. Saturday, March 5, 2011 1 comments

Hivi yesu wa ugenini aliposema msamehe aliyekukosea mara 77alikuwa anamaanisha nini?

Mimi na wewe ni mara ngapi tumesamehe na tukasamehewa?

hivi wewe ukimkuta mme wako anatiana na msaidizi wenu wa wandani wa kike utamsamehe?

hivi kuna makosa ya kusamehe na kuna makosa yasiyo sameheka.

hivi kati ya sheria na msamaha kipi bora?

Posted by nyahbingi worrior. 1 comments

It was a taboo for a black woman to get marred to a whiteman,
It was a taboo for women to dress like the superior(men,i mean black men in africa),
It was a taboo to for a woman to be ipregnated with more than one man,
It was a taboo for a women to eat with the superior in the same table,


unaweza kuendeleza nawe pia.

Posted by nyahbingi worrior. 0 comments

Followers

Popular Posts

Luihamu Ringo